Zaidi ya watoto 100 wameuawa Gaza tangu sitisho la mapigano: UNICEFZaidi ya watoto 100 wameuawa Gaza tangu sitisho la mapigano: UNICEF

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi hii leo ameonteza kuwa “Maisha Gaza bado yanabana na kukosa pumzi. Kuishi bado ni kwa masharti. Wakati mashambulizi ya mabomu na risasi yamepungua, hayajasimama kabisa.”

Kwa mujibu wa UNICEF, kile ambacho dunia inakiita sasa “utulivu” kingechukuliwa kuwa mgogoro mkubwa mahali pengine popote duniani. Lakini kwa bahati mbaya, kusitishwa kwa mapigano kumeleta athari isiyotarajiwa: mateso ya watoto wa Palestina Gaza yameanza kupotea kwenye macho ya dunia.

Kila siku mtoto anauawa

Tangu kusitishwa kwa mapigano, UNICEF imerekodi vifo vya angalau wavulana 60 na wasichana 40 katika Ukanda wa Gaza. Hata hivyo, takwimu hizo zinahusisha tu matukio yaliyokuwa na taarifa kamili, na hivyo idadi halisi ya watoto waliouawa inatarajiwa kuwa kubwa zaidi. 

Msemaji wa UNICEF ameeleza pia mamia ya watoto wengine wamejeruhiwa. “Nilikaa na mmoja wa waathirika hao siku chache zilizopita. Jina lake ni Abid Al Rahman, mtoto mwenye umri wa miaka tisa, alikuwa anakusanya kuni pamoja na marafiki zake huko Khan Younis wakati shambulio la anga lilipowapiga. Vipande vya bomu vilimpasua jicho, kipande hicho cha chuma cha mlipuko bado kimekwama ndani yake,” amesema Elder.

Wakati huohuo, mashambulizi yakiendelea, vikwazo vikubwa bado vinadhibiti upatikanaji wa mahitaji muhimu Gaza kuanzia baadhi ya dawa muhimu, gesi ya kupikia, mafuta ya kuendeshea mashine, hadi vipuri vya mifumo ya maji na usafi wa mazingira inayookoa maisha.

Hatua zilizochukuliwa na UNICEF tangu kusitishwa kwa mapigano

Kusitishwa kwa mapigano kumeruhusu mafanikio muhimu katika maeneo kadhaa ya kibinadamu. UNICEF inataja baadhi ya maeneo hayo ni:

Afya: Kupanua huduma za afya ya msingi na chanjo, hasa kaskazini mwa Gaza ambako hapo awali hakukuwa na huduma.

Maji, usafi na mazingira: Kuondoa hadi tani 1,000 za taka ngumu kila mwezi; kukarabati mabomba ya maji, vituo vya kusukuma maji na mitandao ya maji taka.

Msimu wa baridi: Kusambaza karibu blanketi milioni 1 za joto na mamia ya maelfu ya vifurushi vya nguo za baridi kwa watoto.

Lishe: Kuongeza zaidi ya vituo 70 vya huduma za lishe kote Gaza, hatua iliyosaidia kupunguza hatari ya njaa kali.

Hata kwa mafanikio hayo ya kiasi, miaka miwili ya vita imewaacha watoto wa Gaza katika maisha magumu yasiyoelezeka. Bado wanaishi katika hofu, na majeraha yao ya kisaikolojia hayajatibiwa yakiendelea kuwa makubwa na magumu kupona kadri muda unavyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *