#HABARI: Ujenzi wa mradi wa chujio la maji la mradi wa kuvuna maji ya mvua wa Mwendakulima wilayani Kahama, unaojengwa gharama ya shilingi bilioni 4.8 umefikia asilimia 91.
Akielezea mradi huo ambao unajengwa katika eneo la Mgodi wa Buzwagi, baada ya kufungwa na kubadilishwa kuwa kongani ya viwanda na biashara, msimamizi wa ujenzi wa mradi huo Mhandisi Magige Marwa, amesema kazi inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Februari, 2026 ambapo changamoto ya kukatika maji, wakati chanzo kikuu cha maji ya Ziwa Victoria kinapopata hitilafu itamalizika kabisa.
Naye mwakilishi wa uongozi wa Mgodi wa Barick, ambao umechangia zaidi ya asilimia 50 ya gharama za mradi, amesema ushirikiano kati ya wadau na serikali umechangia kuleta maendeleo ya kasi kwenye jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, ameielezea mradi huo utatatua kero ya muda mrefu ya kukatika katika maji iliyokuwepo na kuitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira, Kahama kuhakikisha mradi huo unatunzwa kwa ajili ya maslahi ya wananchi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania