Dar es Salaam. Wakati wasanii wengine wa kike wakiambatana na wasimamizi wao ambao ni wanawake, katika sehemu mbalimbali za kazi. Hii ni tofauti kwa msanii Aya Nakamura ambaye amekuwa akimruhusu Bodyguard wake wa kiume kumvalisha na kumshika sehemu yoyote.
Katika siku za hivi karibuni, jina la Aya Nakamura, limekuwa likitajwa sana katika mitandao ya kijamii akihusishwa kuwa na ukaribu uliopitiliza na bodyguard wake hata akiwa katika shughuli zake binafsi.
Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, zinaeleza kuwa ukaribu wa bodyguard huyo katika maisha ya Aya unaonekana kuwa zaidi ya jukumu lake la kawaida la ulinzi. Katika baadhi ya matukio, mlinzi huyo amekuwa akiongozana na Aya hata katika safari za faragha, hali iliyowafanya baadhi ya watu kuhoji iwapo uhusiano wao ni wa kikazi pekee au kama kuna jambo jingine zaidi.
Mbali na hayo, taarifa nyingine zinaeleza kuwa Aya amempa bodyguard huyo ruhusa ya kumsaidia kurekebisha mavazi yake pale yanapokuwa hayapo sawa. Vilevile inadaiwa kuwa ukaribu wao umefikia hatua ya kumruhusu mlinzi huyo kumshika sehemu yoyote ya mwili wake, hali inayoongeza maswali kutoka kwa mashabiki.
Kutokana na hatua hiyo mashabiki baadhi wamekuwa wakimpongeza msanii huyo kupata mlinzi anayeweza kumsaidia kila kitu kwani watu maarufu huhitaji walinzi wanaowaamini kwa kiwango cha juu kutokana na changamoto za kiusalama wanazokutana nazo. Hata hivyo wengine walikosoa ukaribu huo wakiuuita ‘ukaribu uliovuka mipaka ya kazi’ huku wakisisitiza huwenda wakawa na mahusiano.
Aidha mpaka kufikia sasa msanii huyo hajaweka wazi kuhusu ukaribu wake na mlinzi wake kama ni ukaribu wa kazi tuu ama mahusiano ya kimapenzi.
Aya Namukura ni nani?
Jina lake halisi ni Aya Coco Danioko, ni mwanamuziki na mtunzi wa nyimbo mwenye asili ya Mali alizaliwa Mei 10, 1995, na kukulia nchini Ufaransa. Aya ni mmoja wa wasanii wa kike waliofanikiwa zaidi barani Ulaya na Afrika kwa muziki wa Afropop, R&B na pop ya Kifaransa.
Umaarufu wake ulipanda zaidi mwaka 2018 baada ya wimbo wake wa “Djadja” kufanya vizuri kimataifa na kufikia mamilioni ya watazamaji kwenye majukwaa ya kuuza na kusikiliza muziki. Baada ya hapo, aliachia vibao vingine vingi vilivyompa heshima kubwa katika tasnia ya muziki, vikiwemo “Copines”, “Pookie” na “Jolie Nana”.