Vikosi vya usalama vimezingira nyumba ya kiongozi wa upinzani nchi Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine.

Bobi Wine ambaye anashiriki katika kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu nchini Uganda ameonyesha upinzani mkubwa dhidi ya Rais Yoweri Museveni anayetetea kiti chake kwa miaka 40 mfululizo.

Mapema leo asubuhi vikosi vya usalama vilizingira nyumba ya kiongozi huyo iliyopo katika mji mkuu wa Kampala.

Taarifa ya chama chake cha National Unity Platform (NUP), imesema vikosi hivyo vimewaweka chini ya ulinzi Bobi Wine na mkewe.

“Mapema asubuhi leo vikosi vya ulinzi na usalama vilifika nyumbani kwa kiongozi wetu (rais wa chama) na kuwaweka kifungoni na kuwaamuru wasitoke ndani..”

Tayari Tume ya Uchaguzi nchini humo imetangaza matokeo ya awali ambapo yanaonyesha Rais Yoweri Museveni anaongoza kwa asilimia zaidi ya 70 huku mtandao wa internet ukiwa umekatwa Katika maeneo yote ya nchi hiyo.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *