#HABARI: Rais wa Chile, Gabriel Boric, ametangaza hali ya janga katika mikoa miwili ambako moto mkubwa wa misituni umesababisha vifo vya takribani watu18.

Zaidi ya watu 50,000 wamehamishwa kutoka kwenye makazi yao katika mikoa ya Ñuble na Biobío, iliyopo takribani umbali wa kilomita 500 kusini mwa mji mkuu, Santiago.

Moto umeteketeza misitu mikavu iliyo karibu na jiji la pwani la Concepción, na kwa mujibu wa Maafisa wa kushughulikia maafa, takribani nyumba 250 zimeharibiwa.

Vyombo vya habari vya ndani vimeonesha picha za magari yaliyoungua na kubaki mabaki barabarani.

Shirika la misitu la Chile, Conaf, lilisema kuwa zimamoto walikuwa wakipambana na moto kote nchini siku ya Jumapili. Moto hatari zaidi, liliongeza, upo katika mikoa ya Ñuble na Biobío.

Moto umeteketeza ekari 21,000 katika mikoa hiyo miwili hadi sasa.
“Kwa kuzingatia uzito wa moto unaoendelea wa misituni, nimeamua kutangaza hali ya janga katika mikoa hiyo miwili,” Rais Gabriel Boric alisema katika ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa X.

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *