#HABARI: Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imezindua ujenzi wa kituo cha “Msichana Center” mjini Bagamoyo, mkoani Pwani, kikiwa ni kituo cha tano cha aina hiyo kuanzishwa nchini. Kituo hicho kinalenga kuwasaidia wasichana kukabiliana na changamoto za ukatili wa kijinsia, huku kikitoa mafunzo yatakayowawezesha kujikwamua kiuchumi na kutimiza ndoto zao za baadaye.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Stellah Msofe, amebainisha kuwa ujenzi wa kituo hicho utagharimu takriban shilingi bilioni nne. Mradi huu unatajwa kuwa mkombozi mkubwa kwa mabinti wa mkoa wa Pwani, kwani utatoa hifadhi salama na mazingira wezesha ya kupata stadi za maisha na ulinzi dhidi ya vitendo vya kikatili.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.