Nigeria. Muziki wa Nigeria umekua kwa kasi na umefika mbali duniani, kwa sasa na wasanii wa nchi hiyo wanajulikana kwa utajiri mkubwa kutokana na umaarufu mkubwa walioupata.

Wasanii hao sio tu wanajivunia umaarufu, pia wanashikilia rekodi ya mapato makubwa, wakiuza mamilioni ya albamu, kufanya ziara za kimataifa na kuingia katika biashara mbalimbali.

Mwananchi inakuletea orodha ya wasanii 10 wa Nigeria walio na utajiri mkubwa zaidi, kulingana na tathmini ya thamani zao na mapato mbalimbali.

MASHE 01

Kwa mujibu wa Truehost, David Adedeji Adeleke maarufu Davido

ndiye msanii tajiri zaidi Nigeria kwa sasa akikadiriwa kuwa na utajiri wa Dola 100 milioni ambayo ni sawa na Bilioni 370 za Kitanzania.

Thamani yake inakadiriwa kuwa dola milioni 100, kutokana na ziara za kimataifa na shoo anazojaza hususan Marekani, mikataba ya matangazo na ushirikiano wa kibiashara.

Davido anamiliki ndege binafsi (private jet), nyumba za kifahari na magari ya gharama kubwa, huku akiwa na biashara kubwa ndani na nje ya muziki wake unaomfanya kuwa na thamani hiyo.

MASHE 02

Nyota huyo anayetamba na kibao cha Jogodo akishirikishwa na Asake anashika nafasi ya pili kwenye chati ya wanamuziki matajiri nchini humo.

Mfalme huyo wa Afrobeat ana thamani ya Dola 65 milioni sawa na Bilioni 240 za Kitanzania, amefikia thamani hiyo kutokana na muziki wake, mikataba ya chapa, ziara za kimataifa na muziki wa Afrobeat unaosikika kote duniani.

Muziki wake umejizolea mamilioni ya Dola, shoo anazopiga Ulaya pamoja na nyumba za kifahari anazoishi na mitindo ya maisha ya kifahari

Inaelezwa kolabo yake na Drake kwenye remix ya wimbo wa Ojuelegba miaka tisa iliyopita ilimtengenezea brandi kubwa kwenye muziki wa kimataifa akapiga shoo za mabilioni ya pesa.

MASHE 03

3. Don Jazzy

Don Jazzy ni mtayarishaji wa muziki na mtunzi maarufu nchini humo ambaye amejizolea umaarufu kupitia kazi zake ikiwemo Overloading ya Mavins, Minding mya Business ya Korede Bello, Anyway ya Johnny Drille na nyinginezo.

Inaelezwa kazi hizo zimemfanya kuwa miongoni mwa watayarishaji wanaopiga pesa nyingi nchini humo na ana utajiri unaokadiriwa kuwa Dola 52 milioni sawa na Bilioni 193.

Anaongoza lebo ya Mavin Records kama prodyuza mkuu akizalisha wasanii wengi maarufu akiwemo Rema, Tiwa Savage, Ayra Starr na wengineo.

Nje ya muziki mapato yake pia yanatokana na uwekezaji wa kibiashara na matangazo ya chapa mbali na uprodyuza.

MASHE 04

4. Burna Boy

Mshindi mara mbili wa tuzo za Grammy, Burnaboy anashikilia nafasi ya nne kwenye chati hiyo akiwa na thamani ya Dola 40 milioni zaidi ya Bilioni 140 za Kitanzania.

Burna Boy ameshinda tuzo mbili za Grammy hadi sasa mwaka

2021 kama Best Global Music Album kwa albamu yake ‘Twice as

Tall’.Hii ilimletea ushindi mkubwa na kumjengea umaarufu kimataifa, akitambuliwa rasmi kama mmoja wa wanamuziki bora wa muziki wa Afrobeat duniani.

Mwaka 2023 pia aliibuka na tuzo ya Best Global Music Performance kwa wimbo wa “Last Last”. Wimbo huo pia ulipata mapokezi makubwa duniani na kumwezesha kupata tuzo nyingine ya Grammy, akiwa msanii wa kwanza wa Afrobeat kushinda katika kipengele hiko.

Mafanikio hayo yamemfanya ajikusanyie utajiri huo kutokana na ziara za kimataifa, mikataba ya matangazo na uuzaji wa albamu.

MASHE 05

5. P-Square

Ni miongoni mwa kundi linalofanya vizuri Nigeria (Peter na Paul Okoye) wanakadiriwa kujikusanyia mamilioni kwa pamoja, na utajiri wao unakadiriwa kuwa Dola milioni 30 sawa na zaidi ya Bilioni 111.

Kwa pamoja mapacha hao wana historia ya ziara kubwa na uuzaji wa albamu ambao umeletea mapato ya mamilioni. Ingawa sasa kila mmoja anafanya kazi kivyake, bado wanabaki kuwa sehemu ya wanamuziki tajiri zaidi nchini.

MASHE 07 (1)

6. Olamide

Olamide ni rapa, mwimbaji,mtunzi wa muziki nchini humo kiufupi maisha yake amewekeza zaidi kwenye tasnia ya muziki.

Olamide, ambaye anajulikana kwa uwezo wake wa kutunga na kuandika mistari ya hip-hop, ameweza kujikusanyia utajiri wa Dola Milioni 25 zaidi ya Bilioni 92.

Anaongoza lebo ya YBNL na amewekeza katika biashara mbali mbali ambazo zimemfanya kuwa na thamani hiyo.

MASHE 07

Inetimi Alfred Odon maarufu Timaya, kwenye listi ya matajiri yuko nafasi ya saba akiwa mmoja wa wasanii wa muziki wa Dancehall wanaoongoza kwa kulipwa mkwanja mrefu.

Utajiri wake unakadiriwa zaidi ya Bilioni 52 za Kitanzania, nje na muziki Timaya amewekeza katika biashara za mafuta na gesi na mali zingine kama nyumba za kifahari na magari.

MASHE 08

8. Flavour

Mwingine ni mfalme wa muziki wa highlife, na utajiri wake unakadiriwa kuwa Dola milioni 10 sawa na Bilioni 37. Amefanikiwa kwa njia ya muziki, matangazo na uwekezaji kwenye mali zingine.

Flavour aliyeanza muziki miaka ya 2005 anatajwa kuwa miongoni mwa wasanii wa muda mrefu wanaopiga pesa kupitia shoo za muziki.

MASHE 09

9. Tiwa Savage

Malkia wa muziki wa R&B na Afrobeat, anashika nafasi ya tisa kwa utajiri mkubwa Nigeria. Ana mapato mengi kutoka katika mikataba ya matangazo, ziara za ndani na nje na muziki wake unaoendelea kutawala Afrika.

Mkali huyo mwenye albamu nne na EP mbili hadi sasa anakadiriwa kuwa na utajiri wa zaidi ya Bilioni 33 akiwa mmoja ya wasanii wa kike wenye utajiri mkubwa.

MASHE 10

Mfalme wa rap na muziki wa hip-hop, amejikusanyia Dola milioni 6.7 sawa na Bilioni 25, thamani hiyo inatokana na  muziki, mapato kutoka kwenye matangazo na miradi mingine ya biashara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *