Rais Masoud Pezeshkian wa Iran ameonya kwamba shambulio lolote dhidi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei litakuwa “vita kamili” na taifa la Iran.

Katika ujumbe wake uliochapishwa kwenye akaunti yake ya X jana Jumapili, Rais Pezeshkian alisema vikwazo visivyo vya kibinadamu vilivyowekwa na Marekani na washirika wake dhidi ya Iran ni moja ya sababu kuu za ugumu wa kiuchumi unaowakabili watu wa Iran.

Jumamosi iliyopita pia, Ayatullah Ali Khamenei alisema Iran inamtambua Rais wa Marekani, Donald Trump, kuwa ni mhusika mkuu wa mauaji na uharibifu uliofanywa na watu wenye uhusiano na mataifa ya kigeni katika ghasia za hivi karibuni.

“Rais wa Marekani anahusika na mauaji, uharibifu na tuhuma za uongo dhidi ya taifa la Iran,” alisema Kiongozi Muadhamu, akimtaja Trump kuwa ni mhalifu.

Baadaye siku hiyo, Trump alikariri kauli yake dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na kutoa wito wa kukomeshwa uongozi wa Ayatullah Ali Khamenei.

Itakumbukwa kuwa, maandamano ya amani ya mwishoni mwa mwezi uliopita nchini Iran yaligeuka kuwa vurugu, huku waandamanaji, waliochochewa na Trump na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na kusaidiwa na mashirika yao ya kijasusi, wakivamia miji ya Iran, kuua askari usalama na raia na kushambulia miundombinu ya umma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *