Mwaka mpya unaashiria mwanzo mpya, matarajio mapya na matumaini mapya ya kesho iliyo bora. Tunapoingia mwaka wa 2026, tunatakiwa kutambua kuwa afya njema ndiyo msingi wa maisha yenye tija, mafanikio na ustawi. Bila kuwa na afya njema hatuwezi ktekeleza kitu chochote na hata mipango ya maendeleo hiwezi kufanikiwa.
Kwa kulitambua hili, Strategis Insurance imeanza mwaka kwa kutoa suluhu la upatikanaji wa huduma za afya kwa urahisi na la gharama nafuu ambalo huweka ustawi wa watu na amani ya akili kwanza, ambalo ni Bima ya Tumaini.
Kuwezesha upatikanaji wa bima ya afya kwa wote
Bima ya Tumaini imeundwa ili kutoa huduma bora za afya kwa gharama nafuu. Kuanzia Sh 100,000 tu, watu binafsi na wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMEs) wanaweza kupata huduma za matibabu zitakazowalinda dhidi ya gharama za huduma za afya zisizotarajiwa.
Bima hii inatoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wanaokuja na kuondoka na wale wanaolazwa, jambo linalohakikisha ulinzi kwa mahitaji ya kila siku ya huduma za afya pamoja na huduma zinazohitaji kulazwa hospitalini.
Kinachoitofautisha Tumaini ni wigo wake mpana kwani bima hii inatoa ulinzi kwa huduma za matibabu kwa wagonjwa wanaokuja na kuondoka na wale wanaolazwa.
Hii ina maana kwamba, wenye bima hii wanalipiwa majhitaji yote ya huduma za afya kama vile huduma za ushauri, vipimo, matibabu ya kawaida, pamoja na matibabu ambayo yanahitaji kulazwa hospitalini.
Kwa kutoa huduma katika mahitaji yote ya huduma za afya, Tumaini inawasaidia wateja kuepuka matatizo ya kifedha ambayo mara nyingi huambatana na gharama za matibabu zisizotarajiwa.
Kuunga mkono malengo ya kitaifa ya afya na maendeleo
Strategis inafanya kazi sambamba na kuunga mkono ajenda ya Serikali ya kuongeza ufikishaji wa bima kwa wananchi na hivyo kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za afya nchini kote.
Akizungumzia kuhusu hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Strategis Insurance- Kitengo cha Bima za Afya, Dk Malav Manek amesisitiza dhamira ya kampuni hiyo kwa kueleza kuwa;
“Tunaunga mkono kwa dhati ajenda ya Serikali ya kufanya bima ya afya ipatikane kwa wote. Bidhaa zetu zimebuniwa ili kusaidia kujenga mustakabali wenye afya na ustahimilivu zaidi kwa watu binafsi na SMEs. Hii ni dhamira yetu kwa ustawi wa Taifa na ukuaji endelevu,” anasema Dk Manek.
Upatikanaji wa urahisi kupitia mtandao mpana wa Strategis Insurance
Moja ya jambo bora kuhusu Bima ya Tumaini ni mtandao wake mpana wa watoa huduma za matibabu. Strategis Insurance inashirikiana na hospitali na vituo vya afya zaidi ya 300 nchini kuhakikisha kuwa wateja wanapata huduma bora za afya popote walipo. Iwe katika vituo vya mijini au maeneo ya pembezoni, wamiliki wa bima hii wanaweza kupata matibabu bila ucheleweshaji usio wa lazima au kusafiri kwa umbali mrefu.
Ufikiaji huu wa nchi nzima unasaidiakuongeza urahisi na Imani kwa wateja, ukiimarisha ahadi ambayo Tumaini inawakilisha sio tu matumaini, lakini usaidizi bora pale unapohitajika.
Kwa nini uchague Bima ya Tumaini?
Tumaini ni zaidi ya jina, ni ahadi kwa wateja kwamba afya na ustawi wao ni kipaumbele chetu. Kwa kuchagua Bima ya Tumaini, wateja watanufaika na faida zifuatazo;
• Huduma kwa wagonjwa wa wasiolazwa na wanaolazwa
• Gharama nafuu kuanzia Sh 100,000 tu
• Kupunguza gharama za matibabu nje ya mfuko
• Ufikiaji wa nchi nzima kupitia matawi ya Strategis na washirika wake
• Inakupa amani ya akili na hivyo kukuwezesha kuzingatia malengo binafsi na ukuaji wa biashara
Ili kuongeza ufikiaji zaidi, Bima ya Tumaini inapatikana katika matawi yote ya Strategis Insurance nchini nzima. Wateja wanaweza pia kupata bima hii kupitia washirika wanaoaminika, zikiwemo benki, madalali wa bima na mawakala wa bima waliosajiliwa.
Mtandao huu mpana wa usambazaji unahakikisha kuwa Tumaini inafikiwa kila wakati, bila kujali wateja wako wapi.
Anza mwaka 2026 kwa kujiamini
Kuanza mwaka 2026 ukiwa na bima ya afya ni uamuzi sahihi kwako. Ni uwekezaji katika mapato yako, familia yako na maisha yako ya baadaye. Kwa bei yake nafuu, huduma za matibabu ya kina na upatikanaji wake nchini nzima, Bima ya Tumaini inakupa njia sahihi ya kuanza mwaka salama.
Wakati mwaka unavyoendelea huku kukiwa na changamoto za hapa na pale, acha Bima ya Tumaini iwe msingi unaokuruhusu kuzingatia kile ambacho ni muhimu katika kukufanya uishi vyema, kutimiza matarajio yako na kujenga kesho yenye afya zaidi.