Nkasi. Wilaya ya Nkasi imeanza kuchukua hatua kuimarisha usalama wa wananchi dhidi ya majanga, baada ya kukamilisha nyaraka muhimu za usimamizi wa maafa zitakazotumika kama mwongozo wa kuzuia na kukabiliana na majanga kabla hayajasababisha madhara.

Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijualikali akizungumza  wakati wa kikao cha Kamati elkezi ya wilaya ya usimamizi wa maafa, amesema nyaraka hizo zitaisaidia wilaya kubadili mwelekeo wa kukabiliana na maafa kwa kujiandaa mapema na kuyazuia.

Mkuu huyo wa wilaya amesema maandalizi hayo ni sehemu ya mkakati wa kulinda maisha ya wananchi, mali zao na miundombinu muhimu, hususan katika maeneo yanayokabiliwa na vihatarishi vya majanga ya asili na yanayosababishwa na binadamu.

Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Peter Lijualikali (kushoto) akifuatilia nyaraka za usimamizi wa maafa wakati wa kikao cha Kamati Elekezi ya Wilaya ya Usimamizi wa Maafa ikihudhuriwa na timu ya wajumbe wa kamati hiyo, Kikao kimefanyika Ukumbi wa Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.

“Elimu na nyaraka hizi zitatupa mwongozo wa mapema wa namna ya kuzuia na kupunguza athari za maafa. Lengo letu ni kuhakikisha wananchi wanakuwa salama kabla majanga hayajatokea,” amesema.

Kwa upande wake, Mratibu wa Maafa Mkoa wa Rukwa, Aziza Kalyatila, amesema uelewa wa masuala ya usimamizi wa maafa ni nyenzo muhimu kwa maendeleo endelevu, akisisitiza kuwa maandalizi ya mapema hupunguza gharama za uokoaji na urejeshaji wa huduma baada ya majanga.

Mratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Roman Paul Mushi akimfafanulia jambo Mkuu wa Polisi wilaya ya Nkasi SSP. Wenceslaus Gumha wakati wa kikao cha Kamati Elekezi ya Wilaya ya Usimamizi wa Maafa ikihudhuriwa na timu ya wajumbe wa kamati hiyo, kikao kilifanyika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.

Kikao hicho kimeandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) na wataalamu wa Halmashauri ya wilaya hiyo, kikilenga kuwajengea uwezo viongozi na watendaji wa wilaya katika kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na maafa.

Ikumbukwe hatua wilaya ya Nkasi kujiimarisha dhidi ya majanga ninutekelezaji wa muongozo mbalimbali iliyopitisbwa na Serikali  kuimarisha maandalizi na uwezo wa taifa katika kukabiliana na maafa na changamoto zitokanazo na mabadiliko ya hali ya hewa, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kupunguza athari zake kwa wananchi na uchumi wa nchi.

Mratibu wa Maafa Mkoa wa Rukwa Aziza Kalyatila aeleza umuhimu wa mafunzo ya masuala ya menejimenti ya maafa kwa mkoa Rukwa wakati wa kikao cha Kamati Elekezi ya Wilaya ya Usimamizi wa Maafa ikihudhuriwa na timu ya wajumbe wa kamati hiyo (hawapo pichani) wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Peter Lijualikali, Kikao kilifanyika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.

Utekelezaji wa miongozo hiyo utaongeza utayari wa nchi katika kukabiliana na maafa, kulinda maisha ya wananchi na kusaidia ustawi wa uchumi, hususan katika kuimarisha uchumi wa kijani unaozingatia mazingira na maendeleo endelevu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *