Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran, Hujjatul Islam Walmuslimin Haj Ali Akbari, amezungumzia matukio ya hivi karibuni na mashambulizi ya maadui kwenye maeneo mbalimbali yakiwemo ya ya kidini na kusisitiza kuwa: Maadui walidhani kwamba wangeweza kulilazimisha taifa la Iran kurudi nyuma na kudhibiti mitaa na viwanja kupitia vitisho na kuzusha hofu, lakini wananchi ambao ndio wamiliki halisi wa nchi hii, walijitokeza kwenye medani na kukabiliiana ipasavyo na fitina hiyo.

Mwanzoni mwa hotuba za Swala ya Ijumaa ya leo, Hujjatul Islam Walmuslimin Haj Ali Akbari amewakumbusha Waislamu umuhimu wa mwezi mtukufu wa Shaaban akisema: Mwezi mtukufu wa Sha’ban ni mojawapo ya fursa bora zaidi katika maisha ya mtu kupata nuru, kutakasa roho, kumridisha mwenyezi Mungu, na kupambwa kwa maadili mema.

Amesema Sha’ban ni mwezi wa rehema za Mwenyezi Mungu na maandalizi ya karamu ya Allah katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, na mwezi wa kuomba msamaha na maghufira.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran alisema: Maelezo mazuri na kamili kuhusu mwezi wa Sha’ban yanapatikana katika Salawat Shabaniyah kwamba Sha’ban ni mwezi wa Mtume Muhammad (SAW), na unahusishwa na mtukufu huyo.

Hujjatul Islam Walmuslimin Haj Ali Akbari amesema: Mtume Mtukufu (SAW) amesema: “Yeyote atakayenisaidia katika mwezi huu atapewa rehema za Mungu,” na kumsaidia Mtume kuna maana ya kuweka mpango wa maisha kwa mujibu wa siira na mienendoi ya Mtume ili baraka na athari za kiroho za mwezi huu ziweze kutimizwa kikamilifu.

Katika sehemu nyingine ya hotuba za Swala ya Ijumaa, Sheikh Haj Ali Akbari amepongeza kazi nzuuri iiliyofanywa na vyombo vya usalama, jeshi, polisi na makundi ya kujitolea ya Basiij katika kuzima njama na mipango ya adui katika machafuko ya hivi karibuni hapa nchini na kusema: Askari usalama, jeshi, na taasisi za kutekeleza sheria, zimeizuia mradi wa adui wa kutekeleza mauaji ya halaiki.

Amesisitiza kuwa jeshi la Waliinmzi wa Mapinduzi ya Kislamu ni nguzo uu ya kulinda wananchi na mapinduzi ya Kiislamu. 

Akizungumzia vitisho vya hivi karibuni dhidi ya taifa la Iran na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema: “Shambulio lolote dhidi ya Kiongozi wa Mapinduzi, ambaye anawakilisha utambulisho wa kitaifa, dini, na taifa la Iran, ni mstari wetu mwekundu na litakabiliwa na jibu la haraka.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *