Awamu ya kwanza ya mradi wa Mabasi yanayotumia Umeme (Zan Bus), imewasili visiwani humo kupitia Bandari ya Malindi, Zanzibar.
Mabasi hayo 10 yaliyowasili jana Jumapili, Januari 24, 2026 yanatarajiwa kuanza kutoa huduma rasmi za usafiri wa abiria Februari, 2026.
Awali akizungumzia mradi huo, Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema unalenga kupunguza msongamano wa magari barabarani pamoja na kuboresha usafiri rafiki wa mazingira Zanzibar.
Kwa mujibu WA Dkt Mwinyi, mradi huo unaotarajiwa kutekelezwa hatua kwa hatua na kuratibiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) na utasimamiwa na Kampuni ya Usafirishaji ya Unitrans kutoka Afrika Kusini.
#StarTvUpdate
(Feed generated with FetchRSS)