Wizara ya Maendeleo ya Vijana imeiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Kagera kufanya uchunguzi wa kina wa madai ya ubadhirifu ikidaiwa kuwa vijana wanaofuga samaki kwa njia ya vizimba katika eneo la Kabunyora kata ya Rulanda walikabidhiwa vifaranga 9,000 badala ya 20,000 huku wakitakiwa kufanya marejesho ya vifaranga 20,000.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Dkt. Joel Nanauka alipokuwa katika ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya vijana mkoani humo.

Mhariri @moseskwindi

#AzamTVUpdates #UTV108

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *