#HABARI: Mahakama Kuu ya Tanzania imeipatia tuzo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kama ishara ya kutambua mchango wake mkubwa katika kutatua migogoro ya wananchi kwa njia ya usuluhishi nje ya Mahakama.

Tuzo hiyo imekabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Bw. Shaibu Ndemanga, kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji, Mhe. Mohamed Usinga, huku ikielezwa kuwa hatua hiyo imesaidia kupunguza mrundikano wa kesi na kuimarisha amani miongoni mwa jamii.

Pamoja na pongezi hizo, Kamati ya Uchumi ya Halmashauri imetoa maagizo kwa ofisi ya Mkurugenzi kuharakisha uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Mji na upimaji wa maeneo ya umma ili kudhibiti uvamizi wa ardhi.

Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, CPA Subira Mgalu, na viongozi wengine wamesisitiza kuwa kukamilika kwa mpango huo ndiyo suluhisho la kudumu litakalomaliza migogoro ya ardhi isiyo ya lazima na kuchochea maendeleo ya mji huo wa kihistoria.

Katika hatua nyingine ya kuimarisha maendeleo, Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji Bagamoyo limepitisha makisio ya bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni 9.9 kwa mwaka wa fedha wa 2026/2027.

Bajeti hiyo inatarajiwa kuwa chachu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati, ukiwemo mpango huo wa upimaji ardhi na uboreshaji wa huduma za kijamii, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya halmashauri hiyo kukuza uchumi na ustawi wa wakazi wa mji huo wa kihistoria.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *