#HABARI: Wananchi wa vitongoji 175 mkoani Mtwara wameipokea kwa shangwe hatua ya Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuanza kutekeleza mradi mkubwa wa kusambaza umeme utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 15.3.
Wakizungumza kwa niaba ya wenzao, wenyeviti wa vijiji vya Mdui na Mnazi wameishukuru Serikali kwa kupeleka mradi huo ambao unatarajiwa kubadilisha maisha ya wananchi kiuchumi na kijamii katika maeneo ya pembezoni mwa mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala, amemtaka mkandarasi kukamilisha kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa kwenye mkataba ili kuepuka usumbufu kwa wananchi.
Meneja Usimamizi wa Miradi ya REA, Mhandisi Deogratius Nagu, amebainisha kuwa mradi huo ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya kufikisha nishati ya umeme katika kila kitongoji, huku mkandarasi akiahidi kutekeleza kazi hiyo kwa weledi na kasi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.