#HABARI: Watu wawili wameuawa na wananchi wenye hasira kali katika Kijiji cha Isalalo, wilayani Mbozi, kwa tuhuma za wizi wa ng’ombe nane wanaodaiwa kuibiwa wilayani Momba.

Katika tukio hilo, wananchi walichoma moto na kuteketeza kabisa gari aina ya Fuso lililokuwa limebeba mifugo hiyo, huku ng’ombe hao wakidaiwa kutoroshwa na watu wasiojulikana mara baada ya vurugu hizo kutokea.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, SACP Augustino Senga, amethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa jeshi hilo linamshikilia dereva wa gari hilo, Kennedy Mwaluvanda, kwa mahojiano zaidi.

Wakati miili ya marehemu ikipelekwa hospitali, polisi wameanzisha msako mkali kuwatafuta watu wengine waliohusika katika wizi huo pamoja na wale waliochukua sheria mkononi, huku wakitoa wito kwa jamii kuacha vitendo vya kujichukulia sheria mkononi.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *