
Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi tisa za Ulaya, pamoja na Kanada na Japan, wamelaani vikali hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kubomoa makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina (UNRWA) katika mji wa Baitul Muqaddas Mashariki unaokaliwa kwa mabavu.
Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi tisa za Ulaya, pamoja na Kanada na Japan, wametoa taarifa, wakisema: “Tunalaani hatua ya Israel ya kubomoa makao makuu ya UNRWA). Hatua hii inaonyesha jaribio la kudhoofisha kazi za shirika hili la kimataifa.”
Sehemu moja ya taarifa hiyo inasema: Tunatoa wito kwa Israel kuacha uharibifu na kuthibitisha tena uungaji mkono wake kamili kwa shughuli za Shirika la UNRWA.
Taarifa hiyo inakuja sikuu chache baada ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kulaani pia kitendo cha vikosi vya utawala wa kizayuni wa Israel cha kubomoa majengo yaliyomo ndani ya eneo la makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina (UNRWA) katika mji wa Baitul Muqaddas Mashariki unaokaliwa kwa mabavu.
Kabla ya hapo pia Francesca Albanese Ripota Maalum wa Umoja wa Mataifa katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu ameilaani Israel kwa kubomoa makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina (UNRWA) katika mji wa Baitul Muqaddas Mashariki unaokaliwa kwa mabavu, na kutaka kusimamishiwa unachama utawala huo wa Kizayuni katika Umoja wa Mataifa.
Huko nyuma pia, Israel ilichukua hatua kama hizo za uadui dhidi ya UNRWA. Mnamo mwaka 2024, Knesset ilipitisha sheria ya kupiga marufuku shughuli za shirika la Umoja wa Mataifa huko Israel, ikidai kwamba baadhi ya wafanyakazi wa UNRWA walihusika katika matukio ya Oktoba 7, 2023, madai ambayo shirika hilo limeyakanusha.