Milio ya risasi ilisikika mapema leo karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa katika mji mkuu wa Niger, Niamey kabla ya hali ya utulivu kurejea.

Video zilizochukuliwa na wakazi wa Niamey karibu na uwanja wa ndege zinaonyesha moshi mkubwa uliotanda angani ulioandamana na sauti ya milipuko huku picha nyingine zikionyesha magari yakiwaka moto.

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dior Hamani katika mji mkuu wa Niger, Niamey una kambi ya jeshi la anga la nchi hiyo na uko umbali wa kilomita 10 kutoka ikulu ya Rais. 

Niger, nchi inayokumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya magenge ya uhalifu yanayobeba silaha, kwa zaidi ya miaka miwili sasa inaongozwa na Abdourahamane Tiani, mkuu wa jeshi aliyempindua rais  aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia mwaka 2023.

Wakazi wa maeneo ya karibu na uwanja wa ndege wa Dior Hamani wameeleza kuwa sauti za risasi zilianza kusikika muda mfupi kabla ya alfajiri ya leo na kwamba hali ya utulivu ilirejea Niamey masaa mawili baadaye. 

Uwanja wa ndege wa Niamey licha ya kuwa na kambi ya jeshi la anga pia una makao makuu ya kikosi cha pamoja kilichoundwa na Niger, Burkina Faso na Mali ili kupambana na makundi ya kigaidi yanayotumbisha amani na kuibua hali ya mchafukoge katika eneo la Sahel. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *