
Timu ya Taifa ya Iran, Team Melli, imetoka sare ya mabao mawili kwa mawili na timu ya taifa ya New Zealand katika mechi ya kundi G iliyopigwa uwanja wa SoFi Stadium huko California.
Ramin Rezaeian, amefunga bao la kwanza la Team Melli na kutengeneza la pili lililowekwa kimiani na Mohammed Mohebi. Kwa New Zealand, mabao yote mawili yamefungwa na Elijah Just, kupitia pasi mbili za Chris Wood.
Katika mechi nyingine ya kundi hilo, Ubelgiji imetoka sare ya 1–1 na Misri katika mchezo uliochezwa jioni ya Juni 15,2026
Misri walipata goli la kwanza kupitia Emam Ashour dakika ya 20. Ubelgiji walisawazisha kupitia goli la kujifunga mwenyewe beki wa Misri, katika kipindi cha pili cha mchezo huo.
Kabla ya hapo Uhispania ilianza kampeni yake ya Kombe la Dunia 2026 kwa kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Cape Verde katika mchezo wa Kundi H.
Matokeo hayo yameifanya kila timu kujikusanyia pointi moja katika msimamo wa kundi hilo, ambalo pia linazijumuisha Saudi Arabia na Uruguay zilizogawana pointi kwa kufungana bao moja kwa moja.
Miamba ya Afrika, Senegal wanaingia dimbani leo kwa ajili ya kunyukana na Ufaransa.. Kila la kheri timu ya Afrika na Iran….