#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Ndugu Jabiri Makame, ametangaza marufuku ya biashara ya Mkaa wa Miti katika Mkoa wa Songwe na kuhimiza matumizi ya Mkaa Mbadala na Nishati Safi ya kupikia ili kulinda mazingira, kunusuru afya za wananchi pamoja na vyanzo vya maji.
RC Makame ameyasema hayo katika Jukwaa la Wadau wa Mazingira, Maji na Nishati Safi ya Kupikia lililoandaliwa ili kujadili na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto za uharibifu wa Mazingira, Misitu, kuhimiza matumizi ya Nishati Safi, utunzaji wa vyanzo vya maji, usafi wa mazingira na udhibiti wa taka ngumu sambamba na mkakati wa uzalishaji wa miche milioni 10, upandaji na utunzaji wa miche inayopandwa.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.