#HABARI: Serikali imeweka mkazo katika kuimarisha ulinzi wa maisha ya wananchi pamoja na mali zao dhidi ya wanyamapori wakali na waharibifu, kama sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kutatua migongano kati ya binadamu na wanyamapori.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamad Hassan Chande, wakati akijibu swali la Mbunge wa Handeni, Mhe. Charles Jacob Sungura (Mb), aliyehoji mikakati ya Serikali katika kukabiliana na changamoto ya tembo wanaoharibu mazao na kuhatarisha maisha ya wananchi katika maeneo ya Mzeli, Sindeni na Kwamatuku.

Mhe. Chande amesema kuwa Serikali tayari imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuweka kituo cha kudumu cha Askari Wanyamapori katika eneo la Handeni kwa lengo la kuongeza mwitikio wa haraka pale yanapotokea matukio ya uvamizi wa wanyamapori wakali na waharibifu.

Aidha, Serikali imeimarisha doria za mara kwa mara, inaendelea kutumia teknolojia za kisasa ikiwemo matumizi ya ndege nyuki (drones) katika kudhibiti mienendo ya wanyamapori, sambamba na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mbinu rafiki za kukabiliana na changamoto hiyo bila kuhatarisha usalama wao.

Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2025/2026, Serikali imeanza kuandaa mwongozo wa kitaifa wa matumizi ya uzio wa umeme unaotumia nishati ya jua pamoja na teknolojia zinazofanana, kwa lengo la kuweka utaratibu bora wa ujenzi wa miundombinu hiyo.

Amesema teknolojia hiyo tayari imeonesha mafanikio makubwa katika nchi kadhaa barani Afrika, na pia hapa nchini katika maeneo yanayopakana na Jumuiya ya Wanyamapori ya Ikorongo, ambako imechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza migongano kati ya wanyamapori na wananchi.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *