#HABARI: Umoja wa Madereva Bodaboda Jijini Mbeya umeiomba Serikali kuingilia kati mgogoro unaofukuta kati yao na Mwenyekiti wa umoja huo, Aliko Fwamba, anayetuhumiwa kushindwa kuitisha Mkutano Mkuu.

Wanachama hao wameeleza kutoridhishwa na uongozi uliopo kutokana na kutojua hali ya mapato na matumizi ya fedha za umoja wao, jambo lililopelekea kuitisha kikao maalum cha kuomba muafaka na uwazi wa kifedha.

Baadhi ya wanachama, akiwemo Lole Fimbo na Michael Mwashilindi, wamesisitiza kuwa kuingilia kati kwa serikali kutasaidia kutatua kero hiyo inayokwamisha ustawi wa umoja wao.

Kwa upande wake, Mwenyekiti Aliko Fwamba amezungumza kwa njia ya simu kutoa ufafanuzi wa upande wake kuhusu malalamiko hayo, huku wanachama wakisubiri suluhu ya kudumu itakayohakikisha usalama wa fedha na umoja wao.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *