
Ulaya ilichukua hatua hiyo wiki iliyopita kwa madai kuwa kikosi hicho, ni sehemu ya kamatakamata iliyofanywa dhidi ya waandamanaji nchini Iran ambao zaidi ya 6000 waliuawa mwezi Januari.
Nchi nyengine ikiwemo Marekani na Canada tayari zilikuwa zimeshakitangaza kikosi hicho kama kundi la kigaidi. Hatua hiyo inazidi kuudhofisha uchumi wa Iran kutokana na vikwazo vyengine vya Kimataifa ilivyowekewa awali.
Iran pia inakabiliwa na vitisho kutoka Marekani kuingiliwa kijeshi, kutokana na mauaji hayo ya waandamanaji inaowataja kuwa wa amani.
Marekani tayari imeshapeleka meli kubwa kabisa ya kijeshi aina ya USS Abraham Lincoln na makombora mengine Mashariki ya Kati tayari kuishambulia Iran. Lakini haijawa wazi iwapo rais Donald Trump atatumia nguvu kiasi gani dhidi ya taifa hilo.