AZAM FC: “Calculator (kikokoto) haituhusu”
Afisa Habari wa Azam FC, @hasheem_ibwe anasema njia ya kutinga hatua ya robo fainali sio nyepesi kutokana na mazingira ya kundi yalivyo ambapo mpaka sasa timu mbili zina alama tisa huku moja ikiwa na alama 12.

Ibwe amesema wao hawana wasiwasi wa kusonga mbele japo amekumbusha kuzidisha dua katika safari hiyo.

Azam FC ipo kundi “B” kwenye Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa pamoja na Wydad AC, Nairobi Union na AS Maniema Union.

#CAFCC #KombeLaShirikishoAfrika

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *