Makumi ya wanajeshi wa Marekani wameuawa katika shambulizi la kulipiza kisasi la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) dhidi ya kambi ya kijeshi ya Marekani jijini Dubai, katika Umoja wa Falme za Kiarabu.

Taarifa ya IRGC imeeleza kuwa, wanajeshi 40 wa Marekani wameangamizwa, huku wengine zaidi ya 70 wakijeruhiwa katika operesheni hiyo ya kulipiza kisasi na kujihami ya vikosi vya Iran.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, operesheni hiyo ya IRGC ya makombora na droni imelenga mkusanyiko wa askari wapatao 160 wa Kikosi cha Marine Corps cha jeshi la Marekani jijini Dubai, ambapo 40 miongoni mwa mwao wameuawa.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Makao Makuu ya Khatam al-Anbia ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), makumi ya vituo vya kijeshi vya Marekani vimelengwa katika mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani za Iran, na kwamba wanajeshi zaidi ya 650 wa Marekani wameuawa au kujeruhiwa kufikia sasa, katika mashambulizi hayo halali ya kulipiza kisasi ya Iran.

Haya yanajiri huku Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akisisitiza kuwa, jibu la Iran la kushambulia kambi za kijeshi za Marekani katika baadhi ya nchi za Ghuba ya Uajemi halipaswi kutambuliwa kuwa ni mashambulizi dhidi ya nchi hizo, bali ni jibu halali dhidi ya chanzo cha uchokozi.

Mapema leo asubuhi, wimbi la 15 la Operesheni Ahadi ya Kweli-4 limeanza kwa jina la msimbo la Yaa Zahra (AS) kwa mashambulizi mseto ya makombora, ndege za kivita zisizo na rubani na operesheni maalumu ya kikosi cha wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu dhidi ya kambi za jeshi la Marekani katika eneo la Magharibi mwa Asia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *