Azimio la pande mbili linalolenga kudhibiti uwezo wa Rais Donald Trump
wa kuanzisha vita nchini Iran limeshindwa katika Bunge la Seneti la Marekani,
huku mgogoro ukiendelea kuongezeka Mashariki ya Kati.

Hatua ya mamlaka ya vita ilikataliwa kwa kura 53 dhidi ya 47 ambayo kwa kiasi kikubwa kilipigwa kwa misingi ya chama. Ingesitisha hatua za kijeshi za
Marekani nchini Iran bila idhini ya bunge.

Wabungue wa chama
cha Democratic wanasema kuwa Trump alichukua hatua ya kuishambulia Iran bila idhini
ya Congress kwa kutoa sababu zinazobadilika za vita. Baadhi ya wa Republican wanasema
watazuia azimio hilo, lakini wanaweza kubadilisha msimamo wao ikiwa vita vitaongezeka.

Huku hayo yakijiri Jeshi la Israel
limefanya mashambulizi mengine dihdi ya mkuu wa Iran Tehran.

“IDF imeanza
wimbi la ziada la mashambulizi yanayolenga miundombinu ya kijeshi ya utawala wa
Iran kote Tehran,” Jeshi la Ulinzi la Israel linasema katika taarifa.

Jeshi hilo
halikutoa maelezo zaidi kuhusu eneo mahususi, lakini inasema maelezo zaidi
yatafuata.

Shirika la habari
la AFP linaripoti kuwa waandishi wake walishuhudia mlipuko mkubwa katika mji
mkuu Jumatano usiku.

Hapo awali, jeshi
la Israel lilitangaza kuwa jeshi lake la anga lilikuwa limekamilisha “mashambulio makubwa” dhidi ya kambi ya mashariki ya Tehran yenye
vituo vya amri na maafisa wa usalama wa ndani.

Soma zaidi:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *