
Mwanahabari kutoka nchini Burundi Sandra Muhoza, ambaye amekuwa akizuiwa tangu Aprili mwaka 2024 na baadaye kuhukumiwa jela miaka minne mwezi Januari, ameachiwa huru.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wakili wake amethibitisha hatua hiyo, baada ya Sandra ambaye analiandikia gazeti la La Nova Burundi, kupewa msamaha na kuruhusiwa kwenda nyumbani siku ya Jumatano.
Wakati alipoonekana Mahakamani mwezi Desemba mwaka uliopita katika mji wa Ngozi, alionekana mdhaifu, alikohukumiwa miaka minne jela kwa kupatikana na hatua ya kudharau mamlaka ya nchi na uchochezi.
Alipewa kifungo hicho baada ya mamlaka kumpata na hatia ya kusambaza taarifa kwenye kundi la Whatsapp kuhusu kuwepo kwa ugawaji wa silaha uliotekelezwa na serikali, kwa mujibu wa shirika la Kimataifa linalotetea wanahahari RSF.
Shirika la RSF ambalo limekuwa likishinikiza kuachiwa kwa mwanahabari huyo, linasema kukamatwa na kufungwa kwake jela ni mwendelezo wa vitendo vya serikali kuwanyanyasa wanahabari nchini Burundi.