Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Lavrov, katika mazungumzo ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Seyed Abbas Araghchi ametangaza wazi kuwa mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran ni kinyume na kanuni za msingi za sheria ya kimataifa.

Kulingana na taarifa ya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB), katika mazungumzo hayo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amewasilisha salamu za rambirambi kufuatia kuuawa kigaidi Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, makamanda wa ngazi za juu jeshini na wananchi wa Iran wakati wa mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na Israel.

Lavrov amesisitiza kuwa mashambulizi hayo sio tu yamekiuka sheria ya kimataifa na hati ya Umoja wa Mataifa, bali yatakuwa na matokeo mabaya kwa usalama wa eneo lote la Asia Magharibi na dunia nzima.

Waziri wa  Mambo ya Nje wa Iran, Araghchi, ametumia fursa hiyo kumshukuru Waziri Lavrov kwa kumpigia simu yake na kumuelezea hali ya sasa, akielezea wazi jinsi Israel na Marekani zinavyotekeleza uhalifu dhidi ya wananchi wa Iran, kwa kushambulia makazi, shule, misikiti, hospitali, na vituo vya msaada na huduma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *