Benini imepoteza zaidi ya wanajeshi wake 14 waliouawa katika shambulio la watu wenye silaha wanaohusishwa na kundi la wanamgambo wa kijihadi la JNIM. Shambulio hilo lilitolea siku ya Jumatano Machi 4 katika mji wa Kofonou, ulioko karibu na Karimama kaskazini mashariki mwa Benin, kilomita chache tu kutoka mpaka na Niger. ?Ni zaidi ya mwaka mmoja tu tangu nchi hiyo ikumbwe na shambulio kubwa kama hilo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Cotonou, Jean-Luc Aplogan

Kundi la wanamgambo wa kijihadi la JNIM wenye mahusiano na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaida limedai kuhusika na mauaji ya wanajeshi 15 kwenye kambi ya kijeshi kaskazini mwa Benin.

Zaidi ya kilomita 750 kaskazini mwa Cotonou, katika wilaya ya Karimama, eneo la mpaka na Niger, ngome ya vikosi vya wanajeshi wa Benin (FAB) lililengwa na watu wenye silaha. Jeshi lilikiri rasmi vifo vya wanajeshi kumi na tano na watano waliojeruhiwa, ambao maisha yao hayako hatarini, kulingana na msemaji wa jeshi.

Hii si mara ya kwanza eneo hili kulengwa. Karimama na viunga vyake ilishuhudia hali ya usalama ikidorora katika siku za nyuma.

Kwa kujibu shambulio hilo, ndege ya kijeshi ilitumwa na kukukabiliana na safu ya washambuliaji waliokwa kwenye pikipiki. Operesheni ya angani iliwaangamiza magaidi wanne na kuharibu pikipiki kadhaa, mfumo wa  usafiri ambao wapiganaji wanapenda kutumia.

Kiwango cha tahadhari kimeongezwa

Kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu (JNIM) lilidai kuhusika na shambulio hilo, likisema katika taarifa kwamba linadhibiti eneo lililolengwa. Toleo hili la matukio lilipinga vikali na mamlaka ya kijeshi ya Benin. “Hawadhibiti chochote kabisa,” afisa wa cheo cha juu ameiambia RFI.

Operesheni za kutafuta washambuliaji hawa zinaendelea katika eneo hilo. Kiwango cha tahadhari kimeongezwa katika ngome zote za jeshi la Benin katika eneo hilo.

Mbali na vifo, jeshi halijawasiliana kuhusu hali halisi ya shambulio hilo, wala kuhusu hatua zinazotarajiwa kama sehemu ya majibu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *