Trump

Chanzo cha picha, Reuters

Rais wa wa Marekani Donald Trump na Waziri
wake wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth wameikosoa hatua ya Uingereza kwa
kukataa vituo vyake vya kijeshi katika eneo
la Mashariki ya Kati kutumiwa kuishambulia Iran.

Trump hapo awali aliangazia kile kinachoendelea
nchini Iran katika hafla iliyofanyika Ikulu ya White House.

Kwa upande wake Hegseth alisema kwa “bahati
mbaya “Uingereza ilikataa ombi letu “kutoka siku ya kwanza”.

“Lakini tulifikia lengo letu. Tulifika
huko, na hiyo sasa ni sehemu ya mpango ambao tunatumia kufanya mashambulizi ya
angani…Ni vikosi zaidi vya wapiganaji, ni uwezo zaidi, ni uwezo wa kujilinda
zaidi, na ni mashasmbulizi ya mara kwa mara,” alisema.

“Kiwango mashabulizi dhidi ya Iran na
Tehran kinakaribia kuongezeka kwa kasi,” alisema.

Hegseth pia alisema Marekani na Israel zinawalenga
wale waliokuwa wakiwakandamiza waandamanaji nchini Iran.

“Kadiri unavyofanya hivyo zaidi, kuharibu
nia na uwezo wao, ndivyo unavyotengeneza fursa kwa watu kusimama kwa
ujasiri,” Hegseth alisema.

Melezo zaidi:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *