Duru za kuaminika zimeiambia Rusia Today kwamba nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi zimeanza mazungumzo ya kujadili suala la kufunga kwa muda kambi za majeshi ya Marekani katika eneo la Asia Magharibi.

Ikivinukuu vyanzo vya kuaminika, Televisheni ya Russia Today imesema mazungumzo hayo yanajadili suala la kufunga kwa muda kambi za majeshi ya Marekani Asia Magharibi ili kuepuka mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Ripoti hiyo inasema, kufungwa kambi za majeshi ya Marekani Magharibi mwa Asia ni moja ya malengo makubwa ya Iran tangu kuanza vita vya Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, mwishoni mwa mwezi uliopita wa Februari.

Kambi za majeshi ya Marekani katika nchi mbalimbali za Asia Magharibi zimekuwa zikishambuliwa vikali na Iran tangu nchi hiyo ilipoanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ikishirikiana na Israel.

Wizara ya Vita ya Marekani jana ilitangaza kuwa mwanajeshi mwingine wa nchi hiyo ameuawa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran kwenye nchi za Mashariki ya Kati.

Ripoti zinasema mwanajeshi huyo alikuwa kifanya kazi kwenye mfumo wa rada wa kistratijia wa kutoa tahadhari ya mapema ya mashambulizi ya Iran ambao ni sehemu muhimu ya mfumo wa ulinzi wa makombora wa Marekani. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *