Dar es Salaam. Siku zote ubunifu huleta upekee.  Hilo linajionesha kwa Jean Jacques Ndjoli mbunifu wa picha kutokea jijini Paris, ambaye amejipa utofauti kwa kupiga picha katika maeneo ya kipekee.

Jean Ndjoli, ni kijana mwenye asili ya Congo ambaye anaishi Paris, nchini France. Amejijengea umaarufu kwa kubadilisha mawazo na maeneo katika muundo wa kisanaa.

Safari yake haikuwa rahisi mwanzo. Alilazimika kuachana na masomo ili afanye kile anachokipenda.

Uamuzi huo ulimfungulia milango katika dunia ya art direction, taaluma inayomfanya aoneshe zaidi uwezo wake katika ubunifu.

Shauku yake ya kufanya ubunifu ilianza mwaka 2013, alipokuwa akijaribu kwa ajili ya kujifurahisha. Hata hivyo, aligundua kuwa ubunifu ndiyo kitu kinachompa furaha. 

Uwezo wake wa kupiga picha za kibunifu kwenye mazingira mbalimbali ya asili na majengo ya kipekee ulimfanya apate nafasi ya kushiriki katika matukio makubwa kama Paris Fashion Week. 

Ndjoli ameshapiga picha kwenye maeneo zaidi ya kumi na moja ikiwemo,

*Luyang Lake, Yanghzou, China, 
*TeamLab Phenomena, Abu Dhabi, UAE
*Incense Village, Hanoï, Vietnam
*Wat Rong Khun, Chiang Rai, Thailand
*Shibuya S Monument, Shibuya, Tokyo
*Sidi Moussa Tannery, Fès, Morocco
*Abrahamic Family House, Abu Dhabi
*Reynisfjara Black Sand Beach, Iceland
*Future Museum, Dubai, UAE
*SeaWorld, Abu Dhabi, UAE
*La Muralla Roja, Calpe, Spain

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *