Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania,TFF Wallace Karia, amepigia chapuo dhana ya “No School, No Play” wakati alipotembelea kituo cha michezo cha Future Stars Academy mkoani Arusha.

Dennis Mwasalanga na taarifa zaidi
Hapa Ni Arusha kwenye kituo cha Future Stars Academy inayowakusanya Vijana wa Rika mbalimbaIi kujifunza masuala ya kimichezo ikiwemo soka. Kituo hiki kipo hapa jijini Arusha kwa Takribani miaka 17 hadi sasa.

Katika ziara hiyo, Karia aliwaasa vijana kuzingatia masomo sambamba na michezo, akisisitiza kuwa nidhamu na elimu ndiyo msingi wa mafanikio ya muda mrefu.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *