
Kiongozi wa tatu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran leo ametoa ujumbe wake wa kwanza baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo akitilia mkazo umuhimu wa mchango wa wananchi na mahudhurio yao katika medani na kusema: Wananchi wanataka kuendelezwa mapambano athirifu na ya kumjutisha adui.
Katika ujumbe huo, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei ametoa shurani zake za dhati kwa wapiganaji shupavu wa Iran ambao wamefunga njia ya uvamizi wa adui na mipango yake ya kutaka kuigawa Iran kwa kutoa vipigo murua kwa maadui. Vilevile amewashukuru wapiganaji wa Kambi ya Muqawama akisema kambi ya Muqawama ni sehemu isiyoweza kutenganishwa na thamani na maadili ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
Amesema katika miaka ya karibuni adui ameanzisha kambi na vituo vya kijeshi na kifedha katika nchi jirani na Iran kwa shabaha ya kudhibiti eneo hili, na kwamba Iran imeshambulia baadhi ya kambi za kijeshi zinazotumiwa na adui na itaendelea kufanya hivyo iwapo italazimu. Amesema nchi jirani na Iran zinapaswa kuainisha wajibu wao kuhusiana na mchokozi anayeshambulia nchi na kuua rai wetu. Sayyid Khamenei amesisitiza kuwa Iran daima imekuwa na ina hamu ya kuimarisha uhusiano mwema na wa kujenga na nchi jirani.
Amesisitiza kuwa wenzo wa kufunga Mlango Bahari wa Hormuz unapaswa kuendelea kutumiwa.
Ayatullah Mojtaba Khamenei amesema medani nyingine za mapambano pia zitafunguliwa iwapo hali ya vita itaendelea, kwa mujibu wa maslahi ya taifa.
Vilevile ameliombea dua ya rehma za Allah taifa la Iran, Umma mzima wa Kiislamu na watu wote wanodhulumiwa hususan katika saa na siku hizi zenye baraka tele za Mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Habari ya ujumbe kamili wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu itakujieni baadaye…