Sitasahau yaliyotukuta kulipa kwa simu Baa!Sitasahau yaliyotukuta kulipa kwa simu Baa!

DAR ES SALAAM; Ucheshi! Mdau ametuandikia ujumbe akielezea kisa kilichomtokea na wenzake maeneo ya Sinza, Dar es Salaam walipoenda kujinafasi kwenye Baa moja huku yeye akiwa ndiye ‘tajiri’ wao.

“Ulipaji wa simu kwa mahitaji mbalimbali ni mzuri sana, ila kuna siku mtandao ulitudhalilisha. Niikuwa na wenzangu pale (anaitaja Baa), tukanywa vya kutosha na kwa kweli tulikuwa kero kwa wateja wengine, kwani tulifanya kila aina ya dharau. Ilikuwa tunatembeza vinywaji hata kwa baadhi ya wateja tusiowajua.

“Ilipofika mida ya saa nane za usiku hivi kuelekea tisa tulikuwa hoi, nikaomba nifanye malipo kwa simu, nikaletewa bili ilikuwa kama Sh 750,000 hivi haikuwa fedha nyingi.

Nikalipa vizuri, ila ujumbe wa malipo ulichelewa kufika kule kwa mpokeaji na kwangu pia haukuwa umerudi.

“Yule mhudumu hakuwa muungwana kila baada ya dakika kadhaa akawa anafoka kwamba sisi matapeli tumekunywa bure, hatuna fedha. Alisema maneno mengi ya dharau, akavuta na wengine waliokuwa pale Baa, zogo likawa kubwa, ikaonekana kama sisi matapeli, hivyo tukawekwa chini kaunta tulikuwa kama nane hivi , ilikuwa aibu.

“Nikipiga huduma kwa wateja kwenye ile kampuni ya simu inasema wahudumu wanashughulikia wateja wengine, watakuhudumia hivi punde. Hakika tulidhalilika sana, lakini baada ya kama dakika 45 tukamwambia Yule mhudumu atazame salio katika simu akafanya hivyo, bado mzigo haukuwa umefika.

“Ila dakika tano tangu aangalie salio ujumbe wa malipo uliingia kwangu nikamuonesha, bahati nzuri naye ukawa umeingia tukawa huru,” ameandika mdau. Je wewe limewahi kukutokea jambo gani?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *