Chanzo cha picha, @iribnews
Ujumbe huo kutoka kwa kiongozi mpya wa Iran Mojtaba Khamenei umesomwa na mtangazaji katika runinga ya taifa ya Iran.
Katika maoni yaliyotafsiriwa na BBC Kiajemi,
Khamenei anasema kwamba “mpango wa kuziba Mlango-Bahari wa Hormuz” bado kinapaswa kutumiwa na Iran.
Ameongeza kuwa Iran ina sera ya “urafiki” na nchi jirani, lakini akawashauri kufunga kambi za Marekani, ambayo anasema Iran itaendelea kuzilenga.
Mojtaba Khamenei aliteuliwa kuwa kiongozi mkuu mpya wa Iran tarehe 8 Machi.
Yeye ndiye mrithi wa babake, Ayatollah Ali Khamenei, ambaye aliuawa katika siku ya kwanza ya vita na Marekani na Iran, tarehe 28 Februari.
Tangu kuteuliwa kwake, hajaonekana kwenye TV ya serikali, na ujumbe wake ulisomwa kwa sauti na mtangazaji.
Mojtaba ni mtoto wa pili wa Ali Khamenei na, ingawa kwa muda mrefu alikuwa anachukuliwa kuwa mmoja wa waliotangulia kumrithi, amekuwa na hali ya chini na ameonekana kuwa na ushawishi kutoka nyuma ya pazia.
Mbali na baba yake, mama na mke wa Mojtaba Khamenei pia waliuawa katika mashambulizi ya Marekani na Israel.
Kituo cha televisheni cha taifa cha Iran kimemtaja kama “mkongwe wa vita vya Ramadhani”, bila kutoa uthibitisho wowote iwapo amejeruhiwa.
Reuters imeripoti kwamba “alijeruhiwa kidogo”, kulingana na afisa wa Iran ambaye hakutajwa jina.