#HABARI: Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado, amesema kuna haja ya wananchi wa Tunduru kuungana bila kujali tofauti za vyama vya siasa ili kuondokana na changamoto za maendeleo zinazoikabili wilaya hiyo.

Ado ameyasema hayo jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vya kati kutoka Tunduru wanaosoma jijini humo.

Amesema Tunduru ni eneo lenye utajiri mkubwa wa kihistoria, kijiografia na kimkakati, lakini bado limekuwa likitajwa kuwa miongoni mwa maeneo yaliyo nyuma katika sekta mbalimbali za maendeleo

Kwa mujibu wa mbunge huyo, katika sekta ya elimu Tunduru imekuwa ikiorodheshwa miongoni mwa wilaya za mwisho katika matokeo ya shule za msingi ndani ya Mkoa wa Ruvuma.

Ameeleza pia kuwa wilaya hiyo haina chuo kikuu, huku akibainisha kuwa hata katika vyuo vya ufundi stadi vya VETA, zaidi ya asilimia 80 ya halmashauri nchini zina vyuo hivyo lakini Tunduru bado iko nyuma kwani ujenzi wa chuo hicho unasuasua na bado haujaanza.

Ado amesema hali hiyo ndiyo iliyompa hamasa ya kuingia katika harakati za uongozi ili kusaidia kuibadilisha Tunduru na kuiondoa katika nafasi za mwisho kwenye sekta mbalimbali.

Amewataka wananchi na wasomi wa Tunduru kushirikiana kwa mshikamano bila kujali tofauti za kisiasa kwa lengo la kuikomboa wilaya hiyo kimaendeleo.

Ado ameahidi kuwa ataongoza kwa vitendo juhudi za kuunganisha wazalendo wa Tunduru wanaoipenda wilaya hiyo na wanaotaka kuona inapiga hatua za maendeleo.

Powered by #MCHEZOSUPA:

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *