#HABARI: Watu wawili wamefariki dunia na wengine wanne wa familia moja wamejeruhiwa baada ya kupigwa na radi wakati mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika Kijiji cha Kilosa mpepo, wilayani Malinyi mkoani Morogoro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama, amewataja waliofariki dunia ni Nindi Masele (15) na Marwa Mwanzilwa (2), wote wakazi wa kijiji hicho.
Ameongeza kuwa waliojeruhiwa ni Milembe Dase (27), Kulwa Malembe (38), Milembe Samwel (39) na Ngolo Nchimwe (1) ambao wanaendelea kupatiwa matibabu.
Hii ni mara ya pili ndani ya mwezi mmoja kwa tukio kama hilo kutokea mkoani humo. Februari 23, 2026, katika kitongoji cha Mbesi, Kijiji na Kata ya Utengule, Halmashauri ya Mlimba, wilayani Kilombero, watu wawili walifariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi.
Mvua hizo pia zimeendelea kusababisha vifo na uharibifu wa miundo mbinu.
Machi 14, 2026, watu wawili wamekufa maji ambao ni Hamis Yahaya Waziri (45), mkulima wa Kisaye, na Nyerere Katebeka Kidagati (50), mfugaji wa Mkono wa Mara, Wilaya ya Morogoro.
Watu hao wamefariki dunia wakijaribu kuvuka sehemu zilizojaa maji na kuwazidi nguvu.
Powered by #MCHEZOSUPA:
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.