#HABARI: Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki, amesema mdahalo wa wadau kuhusu maji na jinsia ni fursa muhimu ya kuhakikisha wanawake, vijana na makundi maalum wanapata upatikanaji wa maji kwa usawa na uendelevu.
“Tunapaswa kuweka mifumo inayowafikia wanawake wenye ulemavu na wale wanaoilea kaya zenye ulemavu, ili kila mmoja apate haki sawa,” alisema Kairuki.
Amesema hayo kwenye mdahalo huo wa Kitaifa uliofanyika mjini Morogoro ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya wiki ya Maji ambayo Kitaifa inafanyika Mjini Morogoro ambayo kwa mwaka huu Ina Kauli mbiu “Rasilimali za Maji na usawa wa kijinsia”.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Maji na Mazingira, Mhe Jackson Kiswaga, amesema Bunge lina jukumu la kuhakikisha sheria na miongozo ya maji zinadumisha usawa wa kijinsia.
Naye Mhandisi Mwajuma Waziri, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, amesema mdahalo huo ni fursa ya wadau kushirikiana na Serikali kuangalia mikakati ya kuboresha upatikanaji wa maji.
Christina Mhando, WaterAid Tanzania, ni mwakilishi wa mashirika ya Kimataifa yaliyoshiriki mdahalo huo anasema huduma bora ya maji huboresha maisha ya wanawake na wasichana, ikipunguza mzigo, kuongeza muda na kuongeza ushiriki wao kikamilifu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Powered by #MCHEZOSUPA:
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.