#HABARI: Wizara ya Maliasili na Utalii, kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wilayani Nanyumbu, imetangaza kuwa uzalishaji wa mazao ya nyuki umeimarika kwa kasi na kufikia zaidi ya kilo 700.
Ongezeko hili la asali na nta linatokana na juhudi za TFS katika kusimamia mazingira ya misitu na kutoa utaalamu kwa wafugaji, jambo linalofanya Nanyumbu kuwa kitovu kipya cha uzalishaji wa asali bora mkoani Mtwara.
Mtaalamu wa ufugaji nyuki kutoka TFS Nanyumbu, Yona Bayo, amebainisha kuwa pamoja na mafanikio hayo, mahitaji ya asali katika soko la ndani na nje ya nchi bado ni makubwa sana kuliko uzalishaji wa sasa.
Hali hii inatoa fursa ya kipekee kwa Watanzania na wawekezaji kuingia katika sekta ya ufugaji nyuki, kwani soko la uhakika lipo na bidhaa hiyo inazidi kutafutwa kwa ajili ya matumizi ya chakula na dawa.
TFS imewahimiza wananchi kuchangamkia fursa hiyo ya kiuchumi kwa kuanzisha miradi ya ufugaji nyuki ambayo haihitaji gharama kubwa za uendeshaji lakini ina faida kubwa.
Aidha, wakala huo umeahidi kuendelea kutoa mwongozo wa kitaalamu ili kuhakikisha uzalishaji unaongezeka zaidi, lengo likiwa ni kukuza kipato cha mwananchi mmoja mmoja na kuongeza mchango wa sekta ya nyuki katika pato la taifa.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.