Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tabora, imesitisha mkutano wa sherehe ya Injili ya Miujiza ambao ulikuwa ufanyike kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Kazembe Manispaa ya Tabora.

Mkutano huo ulipangwa kufanyika March 19 hadi March 22, 2026. Hata hivyo, ilibainika kuwa waandaaji wa mkutano huo walisambaza vipeperushi na vifaa vya michezo ikiwamo mipira kwenye shule 54 za msingi na sekondari vikiwa na alama zinazodaiwa ni za ushoga.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paulo Chacha amesema licha ya kuzuia kufanyika kwa mkutano huo ameagiza Mchungaji Dr. Dana Morey kutoka nchini Marekani na wati alioambatana nao waondoke mkoani huko leo hii ikiwa ni pamoja kuondolewa kwa mabango yote ambayo yamebandikwa katika maeneo mbalimbali ya mji.

Akiongea na vyombo vya Habari na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tabora, Mchungaji Rashidi Iddi ambae ni mwenyeji wa wageni hao amekili kupeleka mpira na mwaliko wa mkutano huo wa Injili kwa Mkuu wa Mkoa, Tabora Chacha bila kufahamu kuwa vifaa hivyo vilikuwa na alama ambazo zinaashiria kuchocjra kwa mapenzi ya jinsia moja.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *