Senegal na Marekani zimesaini mkataba wa afya wa miaka mitano, dola milioni 135 huko Dakar siku ya Ijumaa. Sehemu ya mkakati mpya wa afya wa kimataifa wa utawala wa Trump, unashughulikia nyanja zilizopewa kipaumbele kama vile VVU/UKIMWI, malaria, ufuatiliaji wa magonjwa, na maandalizi kwa magonjwa ya milipuko. Washington itachangia dola milioni 63, huku Dakar ikiwekeza dola milioni 72. Mkataba huo, uliowasilishwa kama ushirikiano wenye usawa, unaibua maswali, hasa kuhusu kushiriki data za afya.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Dakar, Juliette Dubois

Kulingana na serikali ya Senegal, Marekani inachangia dola milioni 63 na Senegal dola milioni 72 kwa kipindi cha miaka mitano, huku Dakar ikichukua hatua kwa hatua majukumu yanayoshughulikiwa na Washington, kama vile usambazaji wa bidhaa za matibabu na ufadhili kwa wafanyakazi wa afya walio mstari wa mbele.

Mkataba huo haujumuishi sehemu ya uhamiaji, kulingana na chanzo katika Wizara ya Afya, tofauti na mikataba mingine kama hiyo iliyosainiwa na nchi zingine za Afrika, ambapo kuwapokea watu waliofukuzwa na Marekani kulikuwa miongoni mwa makubaliano.

Kuhusu data hizo, wizara inabainisha kuwa hakuna rekodi za matibabu za mtu binafsi zitakazosambazwa. Ni takwimu zilizokusanywa pekee zitakazoshirikiwa, ili kuthibitisha kwamba fedha hizo zinatumika kwa ufanisi. Utaratibu wa kawaida, kulingana na wizara.

Suala hilo liliibuka kwa maneno nyeti zaidi nchini Kenya mnamo mwezi Desemba. Washington kisha iliomba ufikiaji wa moja kwa moja kutoka Nairobi kwa data kuhusu vimelea vyenye uwezekano wa magonjwa ya milipuko, taarifa ambazo hapo awali zilikuwa zimesambazwa kwa WHO pekee.

Makubaliano haya ni sehemu ya mkakati wa utawala wa Trump wa “America First Global Health “. Tangu mwezi Januari, Washington imesaini makubaliano kama hayo na nchi zaidi ya kumi na tano za Afrika, ikipita mashirika ya pande nyingi, ikiwa ni pamoja na WHO, ambapo Marekani ilijiondoa rasmi mwezi Januari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *