Ukandamizaji wa Iran pia unazidi kuongezeka. Mkuu wa polisi ametangaza Jumapili jioni kwamba watu 500 wamekamatwa kwa kosa la ujasusi tangu kuanza vita, anaripoti mwandishi wetu huko Tehran, Siavosh Ghazi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na polisi, baadhi ya watu hawa inadaiwa walituma kwa jeshi la Israel viwianishi vya maeneo  ambayo yalishambuliwa baadaye. Wengine walikamatwa kwa kutuma taarifa kwa vituo vya televisheni, haswa Iran International, ambayo hutangaza kutoka nje ya nchi kupitia satelaiti, na vituo vingine vya upinzani, pamoja na video za maeneo yaliyolengwa na mashambulizi wakati wa mashambulizi ya anga, jambo ambalo ni marufuku nchini Iran.

Baadhi pia inasemekana walituma video kwa nchi zingine, ikiwa ni pamoja na Israel, lakini pia kwa Falme za Kiarabu. Kituo cha televisheni cha Iran International, ambacho kinaangaliwa sana nchini Iran, kinachukuliwa na Tehran kuwa tawi la vyombo vya habari la jeshi la Israel na kwa hivyo kinachukuliwa na utawala huo kama adui mkubwa.

Walinzi wa Mapinduzi wamesema kwamba mitambo yote ya satelaiti na miundombinu ya mawasiliano katika nchi jirani zinazotoa huduma kwa chaneli hii sasa italengwa na mashambulizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *