Serikali mkoani Tabora imethibitisha kumshikilia kwa mtu mmoja anaedaiwa kuwa tapeli kwa njia ya mtandao kwa kutumia jina la Waiziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa.
Mtuhumiwa huyo Kange Thabiti 45 mkazi wa Kata ya Kiloleni Manispaa ya Tabora anatuhumiwa kujifanya waziri Mchengerwa na kujaribu kuwatapeli viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali kwa kutumia mawasiliano ya simu na mtandao wa WhatsApp.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paulo Chacha amesema Thabiti alidaiwa kuwasiliana na biongozi hao kwa njia ya simu kabla ya kuwatumia ujumbe kupitia WhatsApp akijitambulisha kuwa ni Waziri wa Afya ili kumshawishi kiongozi huyo aamini kuwa alikuwa akizungumza na kiongozi wa Serikali.
Chacha amesema mtuhumiwa huyo aliweka picha ya waziri Mchengerwa katika akaunti yake ya WhatsApp kama picha ya profile (wasifu) ili kuongeza uhalisia wa mawasiliano hayo na kumfanya mhusika aliyekuwa akizungumza naye aamini kuwa alikuwa waziri huyo.
Aidha, mmuhumiwa alimtaka kiongozi huyo kuhakikisha anatarubu zoezi la kikusanua michango ya harusi haraka na kutumwa kupitia namba ya simu aliyokuwa ameitoa, akisisitiza kuwa maandalizi ya harusi yalikuwa yanaendelea na mchango huo ulikuwa muhimu.
Inadiwa kuwa mtuhumiwa alikuwal akitoa maelekezo bila kufuata itifaki jambo liloibua shaka na kumlazimu kiongozi huyo kuwasiliana moja kwa moja na waziri husika ili kuthibitisha ukweli wa ujumbe aliokuwa ameupokea jambo alilokana kuhusika.
Mtuhumiwa huyo kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi za kisheria ikiwemo kumfikisha Mahakamani kwa ajili ya kujibu tuhuma ambazo zinamkabili.
(Feed generated with FetchRSS)