#HABARI: Serikali imeingilia kati mgogoro wa umiliki wa ardhi unaohusisha wawekezaji wa kigeni katika Sekta ya Utalii wilayani Arumeru, mkoani Arusha, kwa kutuma timu ya wataalamu wa ardhi kufanya uhakiki wa mipaka.

Hatua hiyo inalenga kupata uhalisia wa eneo husika na kuwezesha kutolewa kwa maamuzi sahihi yatakayomaliza mvutano huo na kurejesha utulivu katika shughuli za uwekezaji mkoani humo.

Wakili wa kampuni ya Ker & Downey Safaris Limited (KDT), Bw. Asubuhi Yoyo, amebainisha kuwa mgogoro huo unahusisha kampuni yake na kampuni nyingine jirani iliyopo katika eneo hilo la uwekezaji.

Ameeleza kuwa kuanza kwa mchakato huo wa uhakiki wa mipaka kumeanza kutoa ufafanuzi wa kisheria na kiufundi, jambo ambalo linaashiria kupatikana kwa suluhu ya kudumu ya mgogoro huo uliodumu kwa muda.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *