#HABARI: Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limezindua rasmi matumizi ya ndege nyuki (drones) ili kuboresha ukaguzi wa miundombinu ya umeme nchini.
Hatua hiyo ni sehemu ya mikakati ya shirika kutumia teknolojia ya kisasa katika kuboresha huduma zake.
Matumizi ya drones yatarahisisha utambuzi wa haraka wa hitilafu, hasa katika maeneo ya milima au misitu ambapo ni vigumu kufika kwa miguu.
Hii itapunguza muda unaotumika kutafuta matatizo kwenye nyaya na nguzo za umeme.
Lengo kuu la teknolojia hii ni kuhakikisha Watanzania wanapata umeme wa uhakika wakati wote.
Kupitia mfumo huo, TANESCO itaweza kuzuia hitilafu kabla hazijaleta athari kubwa na hivyo kuimarisha upatikanaji wa nishati nchi nzima.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania