#HABARI: Wanafunzi watatu wa Shule ya Msingi Msongola wilayani Ilala, Dar es Salaam, wamepoteza maisha na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi majira ya saa tano asubuhi ya Machi 18, 2026.
Waliopoteza maisha ni Alexander Paul, Ally Pongwe na Hudhaifa Shafii, huku majeruhi Nadri Maneno na Mahadi Ramadhan wakikimbizwa hospitalini kwa matibabu ya dharura kufuatia tukio hilo la kusikitisha lililotokea katika eneo la Msongola.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linafanya uchunguzi wa mauaji ya Athumani Nyanza, aliyekutwa ameuawa na kufukiwa kwenye shimo kando ya nyumba yake katika mtaa wa Kimya kimya, Zingiziwa.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.