#HABARI:Jeshi la Polisi Kikosi cha Reli Tanzania, linawashikilia watu sabini na saba kwa tuhuma za kuhusika na makosa mbalimbali ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi, kuhujumu miundombinu ya reli, wizi wa mali za shirika kwa kukutwa na vitu mbalimbali ikiwemo shehena ya mafuta na vifaa vinavyotumika katika shughuli za ujenzi wa reli ya kisasa SGR.
Taarifa ya kukamatwa wa watuhumiwa hao pamoja na vitu hivyo, imetolewa na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Reli Tanzania Kamishna Msaidizi wa Polisi Matride Kuyeto wakati akizungumza na vyombo vya habari mkoani Mwanza, ambapo amesema watu hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha, Kamanda Kuyeto amesema miongoni mwa vitu pia vilivyokamatwa ni vilivyokuwa vikitumika katika ujenzi wa kipande cha tano cha SGR Mwanza-Isaka, ikiwemo shehena ya zaidi ya lita 200 za mafuta Pamoja na vifaa vingine ikiwemo nondo.
#MWANZA
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.