#HABARI: Lori la mizigo limeteketea kwa moto katika eneo la Lugono, kando ya barabara kuu ya Iringa–Morogoro, usiku wa kuamkia leo huku mtu mmoja aliyekuwa ndani ya gari hilo akihofiwa kupoteza maisha.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, moto ulianza ghafla na kusababisha taharuki miongoni mwa watumiaji wa barabara hiyo pamoja na wakazi wa maeneo ya jirani.
Sehemu ya kichwa cha lori iliteketea kabisa kabla ya jitihada za uokoaji kuanza.
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji walifika eneo la tukio kwa wakati na kufanikiwa kudhibiti moto huo, hatua iliyosaidia kuzuia madhara zaidi kwa watumiaji wengine wa barabara.
ITV inaendelea kufanya jitihada za kuwapata wasemaji wa mamlaka zingine ikiwemo Jeshi la Polisi kuzungumzia chanzo cha ajali hiyo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.