#HABARI: Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema hakuwa na taarifa mapema kuhusu shambulio la Israel dhidi ya eneo la gesi la Iran, akibainisha kuwa shambulio hilo lililenga sehemu ndogo licha ya hali ya mvutano mkubwa wa kijeshi.
Kupitia ujumbe wake, Trump amesisitiza kuwa wala Marekani wala Qatar hawakuwa na taarifa ya operesheni hiyo, na ameionya Israel kusitisha mara moja mashambulizi dhidi ya miundombinu ya nishati, akieleza kuwa yanaweza kusababisha athari kubwa kiuchumi duniani.
Trump meitaka Iran kuacha mashambulizi dhidi ya Saudi Arabia, Qatar na United Arab Emirates, akisema mataifa hayo hayakuhusika wala kufahamishwa kuhusu shambulio lililotajwa.
Kauli hiyo imekuja baada ya Iran kuripotiwa kufanya mashambulizi makubwa dhidi ya Saudi Arabia, Qatar na UAE usiku wa kuamkia leo, hatua inayoongeza wasiwasi wa kuongezeka kwa mzozo wa kikanda na athari zake kwa usalama wa nishati duniani.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.